journal mama Vision

Bulletin d’information du Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix, RFDP
72, av. Maniema, Bukavu, RDCongo , E-mail :rfdp1999@yahoo.fr , Tél. : +243 (0)813181854, 97783353

N° 000 du 31 mars 2005

Wanawake wa Kivu ya Kusini waomba usalama utekelezwe na wanahakikisha nia yao ya kushiriki katika uchaguzi ujao inchini Congo ya kidemokrasia
Mwanamke, usalama, haki na uchaguzi. Mada hayo manne ndiyo yalikuwa kichwa cha maneno waliyozungumuzia wanawake wa jimbo la Kivu ya Kusini, wakati walipoandamana kwa ajili ya sherehe za sikukuu ulimwenguni ya mwanamke mwaka huu wa 2005, kupitia vyombo mbalimbali vya habari na vya mawasiliano. ( soma ukarasa wa 2-4)

Editorial
Karibu Mama ! (1)

Voici apparaître « MamaVision ».En véritable, elle vous remercie de lui réserver un accueil chaleureux en l’approchant par un « yambi mama... »
et vous suggère de bien vouloir vous asseoir et lui prêter oreille. Question
de s’expliquer en décomposant sa propre dénomination

D’abord « mama ». Autrement dit « maman » en français, ou encore « mère ». Je suis donc une femme. Je sais que vous l’avez bien remarqué en un clin d’oeil, je ne fais que le confirmer. Pour vous rassurer. En même temps, je suis cette fille qui, nourrisson ou adolescente, aspire à la maternité. Une maternité comprise dans le sens d’élever, d’éduquer et
non dans son sens classique d’accoucher, et accoucher seulement.

Ensuite « vision ». Ma double qualité de personne humaine et de maman suppose que j’en ai une. A défaut, je stagnerais et m’écroulerais, emportant avec moi -malheureusement - la famille et la communauté. Ma vision est une vision de moi-même et celle de mon environnement. Elle est fondée sur la construction d’un monde où règnent la paix, la justice, l’équité et la collaboration entre les hommes et les femmes sans aucune forme de discrimination.

Enfin « Mama Vision » est tout simplement une vision de changement. La transformation positive et intelligente de la société pour que la femme change et change son environnement pour le meilleur d’elle-même et de tous.
La survie ainsi que la marche en avant de la famille et de la communauté en dépendent.
Karibu Mama !…., yambi…
Venantie BISIMWA Nabintu
(1) bienvenue maman

Contenu

Wanawake wa Kivu ya Kusini waomba
usalama 2-4

Wanawake wa Kivu ya Kusini waomba
uchaguzi 5

Malalamiko ya wanawake wa Walungu kwa MONUC 6

Proposition d’un projet de loi pour la repression des infractions de violences sexuelles 9

Plaidoyer des femmes du Sud-Kivu 12-14

TUKIO MAALUM
WANAWAKE WA KIVU YA KUSINI WAOMBA USALAMA

Maandamano iliyo fanyika katika mitaa zote za jimbo, iliweza kukusanya umati wa wanawake kutoka pande zote, mjini kama vijijini.
Kabla ya maandamano kamili iliyofanyika mnamo tarehe 8 machi 2005, shirika RFDP (Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et de la Paix), ao (mfumo wa wanawake kwa ajili ya kutetea haki na amani), liliwatembelea wanawake wa mkoa wa Kaniola, mtaani Walungu. Shabaha ya matembezi hayo ilikusudia kukutanisha wanawake hao na viongozi wa serkali na wale wa MONUC (Mission des Nations Unies au Congo) ao Wachunguzi wa umoja wa mataifa inchini Congo. Ili wazungumuze pamoja kuhusu matatizo mengi inayo kumba raia wa mkoa huo, na hasa wanawake ambao wanaendelea kutendewa kinyama usiku kucha na wanamgambo wanyarwanda.

Mawasiliano kamili ilifanyika mnamo tarehe 4 machi katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Kaniola mbele ya umati wa watu, wengi kati yao wakiwa wanawake. Vikundi mbalimbali vya wanawake wa mtaa wa Walungu, na kwa upekee wa mkoa wa Kaniola vilipewa hivi nafasi ya kutoa malalamiko yao kuhusu hali wanayo ishi siku hizi. Ni kama vile CAP (Comité d’Alerte pour la Paix) ya RFDP/Walungu, Mamans Paroisse Kaniola, Mamans Mwangaza, SODEKA, PDFD, RHUZUSANYE, UDEMWA, CODI, CODIBU, TULUKI, AES / IZEGE, NYAMULISA.
Serikali ya Congo ilkuwa ikiwakilishwa na bwana Freddy Masheka, ambaye ni kiongozi makamu wa mtaa mwenyi kuhusika na uchumi na fedha, na MONUC ikiwa na wanawake 6, wakiongozwa na bibi Sylvie, ambaye anahusika na mambo ya upashaji habari na mawasiliano kwenyi kituo cha MONUC cha Bukavu.

Neno lililorudiliwa mara nyingi na wasemaji hao ni lenyi kugusia hasa usalama mkoani humo. Ni kama vile ujeuri, ubakaji, uporaji wa mali ya mlimo, ya ufugo, na mavazi, na vitu vya nyumbani, na hasa uchuruzi wa watu unaovuma siku hizi sehemu zile za inchi.
Matendo hayo huendeshwa na wana mgambo wanyarwanda wa FDLR-Rasta-Interahamwe-Ex –FAR wenyi kujificha ndani ya pori za kando kando za vijiji hivyo. Neno la uzito zaidi ni kwamba baada ya kukamata watu na kuwapeleka porini, wamoja kati yao huchinjwa kwa visu ao kwa mipanga. Wakati wengine hupigwa bila kipimo, wanawake na mabinti wadogo hubakwa ovyo. Baadaye wanawarudisha wamoja kati yao nyumbani, kwa ajili ya kuleta pesa zitakazowagomboa wenziwe. Kaniola, bei ya mutu mmoja ni dollars 100. Pasipo malipo hiyo, mutu hupoteza maisha yake kwa kuchinjwa na kutupwa porini na wanamgambo wanyarwanda pamoja na washiriki wao wakongomani.

Kwa jumla, wanawake waliomba kupitia hotuba mbalimbali walilozitamka usalama utekelezwe mtaani mwao, ili waweze kurudi maskani mwao (kwani yapata elfu 5 ya watu kutoka sehemu hizo ni wahami wanaoishi katika uwanja wa mupira Mafundwe huko Walungu Centre). Walitia mkazo zaidi juu ya kuporwa silaha kwa wanamgambo hao, na kurudishwa kwa usalama wa kudumu inchini mwetu, na pia mtaani wa Walungu. Walishurtisha MONUC iendeshe operesheni hiyo haraka iwezekanavyo sambamba na FARDC, kusudi wapate kushiriki kwenyi uchaguzi ujao.

Kwa ngambo yake, bibi Sylvie toka MONUC, aliahidi wahuzuriaji ya kama atafikisha malalamiko yao kwa viongozi wa MONUC. Ila aliongeza ya kama MONUC, haiwezi kuendesha mapigano sasa hivi na wanamgambo hao. Alifasiria kama wanamgambo hao ni kama nyoka iliyojificha katika kundi la watu. Na kama ukitaka kuishambulia, kutauwawa kwanza watu ambao anajifisha kati yao. Neno hili lilisisimua wanawake ambao walilalamika kama ni sherti MONUC iendeshe operesheni hiyo, kama vile inavyowasaka wanamgambo wa ITURI. Wanawake walipendekeza FARDC ipewe basi vifaa vya lazima na ruhusa ya kuwafuatilia warugarugu hao porini ikiwa MONUC anajuta ao hawezi kuendesha operesheni hiyo. (Mengi kuhusu malalamiko ya wanawake, tunawaalika kusoma hotuba ya wanawake wa kamati ya CAP / Walungu katika ukarasa wa 6.

TUKIO MAALUM

WANAWAKE WANAOMBA HAKI NA USALAMA VITEKELEZWE

Hata kama maneno haya mawili yaligusiwa sana na wanawake wa vijiji vya mtaa wa Walungu mnamo tarehe 4 machi huko Kaniola, usalama na haki iligusiwa kwa namna ya pekee katika mikutano nyingine kuhusu sherehe ya sikukuu ya mwanamke ulimwenguni.
Katika ukumbi wa salle Concordia pa Bukavu, vikundi mbali mbali vya wanawake wa jimbo mzima vilivyo alikwa na ushirika Caucus des femmes du Sud-Kivu pour la paix (ao mkusanyo wa wanawake wa jimbo la Kivu ya Kusini kwa ajili ya amani) pamoja na FPC (Comité Provincial des Femmes) ao Kamati Jimboni ya Wanawake yenyi kusimamiwa na chumba jimboni cha mambo ya maanamke na jamaa (Division provinciale femme et famille), mnamo tarehe 7 machi 2005. Kati ya waalikwa, kulikuwemo pia waimbaji (wanawake, wanaumena pia watoto), ambao walidumbwiza kwa nyimbo na michezo sikukuu hiyo. Kupitia nyimbo za kuomba usalama urudishwe na kutekelezwa kwetu, na kuomba pia sheria ifanye kazi yake ili watenda maovu waazibiwe. Kwani ni njia ya kukomesha vitendo vingi vinavyo angamiza jamii yetu siku hizi.

Katika hotuba aliyotamka kwa niaba ya washiriki kwenyi sikukuu hiyo ya kubadilishiana fikra kuhusu matokeo ya uzito wa vitendo vya ubakaji dhidi ya mwanamke, bibi Zita KAVUNGIRWA, ambaye ni kiongozi jimboni wa Caucus des femmes du Sud-Kivu pour la paix, aligusia maneno haya mawili :
Neno la kwanza ni kwamba kipengele cha 17 cha katiba ya mpito nchini mwetu inatambua ya kwamba watu wote wanayo haki sawa sawa. Neno la pili ni kwamba wanawake wanapashwa kushiriki wote katika uongozi wa inchi kupitia njia ya uchaguzi.
Kwa niaba ya wanawake wa jimbo la Kivu ya Kusini, na wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa jumla, bibi ZITA alionyesha ya kwamba yapata asilimia 53 ya raia wa Congo, ni wanawake. Aliendelea kusema kama wanawake wanapashwa kujiunga, ili uwingi wanao dhidi ya wanaume uwafaidishe, pia nchi nzima pamoja na wanainchi wake wapate faida kupitia kazi za mwanamke. Alishawishi wengine wanawake washiriki katika vyama vya kisiasa kwani ndiyo njia itakayowapeleka kwenyi viti mbali mbali vya uongozi kupitia uchaguzi.

Msemaji aliwaalika wanawake wakongomani wasiambatane tena na tabia ya hapo zamani. Kwani, alieleza, wanawake walikuwa wakishiriki katika vyama vya siasa kwa ajili ya kuwachezea wanaume tu, kuwapigia vigelegele hata kama wanasema uongo na kuwapangiya meza. Mpaka kujigeuza kama makahaba zao. Siku hizi, mwanamke anapashwa kuingia katika siasa kwa ajili ya kugombea kiti cha uongozi. Kwani ana ujuzi na nia nzuri ya kutengeneza inchi hii. Wanawake wanapashwa kuwakilishwa kwa kiasi kwa asimia 30 kwenyi ofisi za hesabu za watu watakaochagua, aliendelea kusema mama ZITA. Kwani Congo inapashwa kujipatia viongozi wazuri ambao watakinga mwanamke pamoja na raia wote kwa jumla, alimaliza msemaji.

Alipochukua usemi, bibi Asseta OUEDRAOGO, mwenyi kuhusika na mambo ya jinsia kwenyi MONUC, alionyesha matatizo wanazo wanawake wa ulimwengu mzima kwa ajili ya kushirikishwa kwa namna inavyofaa katika uchaguzi. Aligusia kwa undani namna jamii huendelea kumgandamiza mwanamke. Alitoa mwaliko kwa wanamemba wa jamii yetu washirikiane ili kufanyike mageuzo dhidi ya wanawake na wanaume wote pamoja. Ni sherti mwanamke awe na urahisi wa kufikilia pia vyombo vya habari na vya mawasiliano. Kwani ni sherti pia usawa wa hali ya wanawake na wanaume ukamilishwe kama inavyo kusudiwa na vyombo vya sheria vya inchi yetu, hata na vya ulimwengu mzima.

Marie Noëlle CIKURU na Laetitia SHINDANO, kutoka katika mashirika Centre OLAME na RFDP, walizungumzia moja kwa moja kuhusu uzito wa ubakaji wa wanawake na wabinti katika jimbo letu na kupendekeza njia za kukomesha vitendo vile kupitia vyombo vya sheria.

TUKIO MAALUM

WANAWAKE WAOMBA HAKI NA USALAMA (futanisho la uk. wa 3)

Alipofungua kipindi hiki, binti Marie Noelle CIKURU (Centre Olame), alionyesha kama tokea mwaka 1995 hadi sasa, mada za sikuu ulimwenguni ya mwanamke hugusia tu usalama na amani. Lakini usalama wa mwanamke huendelea kuzorota siku baada ya siku. Alifanya mzunguko wa jimbo mzima la Kivu ya Kusini na kuonyesha kama vitendo vya ubakaji, uchuruzi wa watu pamoja na mateso ya kila aina vinaendelea kujitokeza bila serkali kufanya lolote. Alieleza kama Centre Olame ilipokea wanawake 330 wahanga wa ubakaji katika kipindi kifupi cha mwezi wa kwanza na wa pili 2005.

Bibi Laetitia SHINDANO, wa shirika RFDP, alipofasiria ukomo wa shirika lake ambalo ni la kutetea haki za binaadamu na amani, alionyesha kama halikubaki kimya mbele ya matatizo ya nyakati hizi zinazokumba wanawake wa Kivu ya Kusini, na hasa wale wa mtaa wa Walungu ambako kunaendeshwa vitendo vyenyi kuleta usalama mdogo na wanamgambo wanyarwanda, pamoja na washiriki wao, wakiwemo watoto wa inchi. .

Kufuatana na hiyo, RFDP inahudumia wahanga wa ubakaji, kupitia uhimizaji wa wahusika wote humu inchini na pia ulimwenguni. Matokeo ya kazi zile zinazoendeshwa na RFDP ni uwepo wa misaada kwa wahanga kama vile kuwapeleka kwenyi vituo vya afya. Kuna pia muundo wa vikundi vyenyi kulenga ukomeshaji wa ubakaji, kama vile CCVS/RDC (Coalition Contre les Violences Sexuelles en RDC) ao mkusanyiko kwa ajili ya kukomesha ubakaji inchini Congo.

Namna gani ubakaji waweza kukomeshwa huku kwetu wakati ambao watu wenyi kuendesha vitendo vile hawajaazibiwa bado na vyombo vya sheria vya humu inchini na vya ulimwengu kwa jumla ? Hili ndilo ulizo ambalo linarudi kila siku midomni mwa raia, na wala halijapata bado jibu. Shirika RFDP lilijaribu kujibia kwa ulizo hili likionyesha waziwazi ya kama kuachilia huru wabakaji ni jambo la kuwapa juhudi ili waendeleshe kitendo kile. Ndio maana linaendelea kutetea kwa bidiii na kupitia ngazi mbali mbali kusudi wabakaji wanao julikana huku kwetu wapate kupelekwa haraka iwezekanavyo mahakamani na wahukumiwe vikali kulingana na sheria. Vile vile linawatetea wamama wahanga wapewe wala warudishiwe haki zao.

Kulingana na mpango huo, CCVS anamoshiriki RFDP iliisha tayarisha mradi mmoja wa kurekebisha na kuongeza sheria kuhusu hukumu wanayostahili wabakaji. Mawazo hiyo ilitokana na kwamba wataalam wa shirika hilo walitambua ya kwamba sheria ya inchi yetu haitambue kitendo cha ubakaji kwa namna inavyofaa, ili pia iweze kuazibu kitendo kile. Azimio la CCVS kuhusu ubakaji ni hakika mojawapo ya njia za kukomesha ubakaji huku kwetu. Kwa sasa, inangojelewa bunge la mpito lichungue mradi huo na kuutangaza rasmi kama sheria.

Hali waishimo wahanga wa ujeuri kulingana na kitendo walichotendewa huzorotesha maisha yao siku baada ya siku. Wanateswa na kuumizwa mwilini mwao kama vile rohoni. CCVS ilitayarisha mradi mwengine wa sheria inayolenga uundaji wa kiwango cha pesa humu inchini kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa ubakaji. Ni wajibu wetu kama wanainchi kuungana na kushurtisha viongozi wa inchi ili mipango hiyo miwili ya kibinadamu ya CCVS ipate kukubaliwa. Wahusika mbalimbali kutoka shirika la raia na za kiserikali inchini mwetu hata na wa umoja wa mataifa walikwisha toa maoni yao kuhusu miradi hiyo.

Kama tunavyotambua, miradi hiyo miwili ambayo hupatikana moja kwa moja bungeni hufafanua kwa kifupi njia linalozitumia shirika RFDP kwa ajili ya kukomesha ubakaji kupitia vyombo vya sheria pamoja na kuwasaidia wahanga wa ujeuri

TUKIO MAALUM

WANAWAKE WAOMBA UCHAGUZI UFANYIKE HARAKA

Maandamano ya sikukuu ulimwenguni ya mwanamke hushuhudia bila shaka ombi rasmi la wanawake wa Kivu ya Kusini ili uchaguzi ufanyike haraka humu inchini kama inavyokusudiwa na katiba yetu ya mpito na pia na walio wengi kati ya raia wakongomani. Mnamo siku ile, umati wa wanawake wasioweza hesabiwa kwa ajili ya uwingi wao walimiminika kutoka pande zote inne za mji wa Bukavu. Ilionekana kama walipendelea kuiheshimisha sikukuu iliyo yao. Na kupitia sikukuu ile, kupata fursa ya kutoa malalamiko yao fulani kwa viongozi wa inchi na kwa jamii kwa jumla. Kati ya vikundi mabalimbali vilivyosherehekea siku ile toka nafasi Christophe Munzihirwa pa Nyawera hadi Place de l’Indépandance, kulikuwemo wanawake wafanya kazi ya serikali, wafanya biashara, wanawake askari na askari polisi, wanawake wabeba mizigo, wanawake wa viama vya kisiasa, wanawake wakulima, wanawake wawakilishi wa mashirika za kiraia za hapa nyumbani na wale wa mashirika za maendeleo za ugenini, wamama toka dini mbalimbali,…

Kupitia nyimbo walizokuwa wakiziimba njiani, vitambaa na vibao, mchezo ulioendeshwa na kikundi Mtu Ni Mtu, wanawake wa Bukavu walikuwa na ujumbe kama huu : « Tunataka amani », « Tunaomba vita Vikomeshwe », « Wabakaji waazibiwe ». Hizi ni kama shurti ambazo zitawaruhusu wanawake kushiriki bila tatizo kwenyi uchaguzi utakaofanyika inchini kama walivyosema wao wenyewe.

Kupitia hotuba, michezo na nyimbo, wanawake wa Bukavu walihakikisha kama wengi kati yao watagombea viti mbalimbali vya uongozi kwa njia ya uchaguzi. Wana aminia uwingi wao. Na pia umoja kati yao. Nia yao hasa ni ya kujenga Congo nyipya ambamo mwanamke na mwanaume wanashiriakiana katika kazi zote bila kubaguana.

HAKI ZA WANAWAKE ZAENDELEA KUKIUKWA MTAANI WALUNGU

Askari mmoja wa FARDC anayejulikana kwa jina maarufu « TEKWA SANS BLAGUE » alimufyatulia risasi binti Pascasie NSIMIRE wa umri wa miaka 20 pa Burhale mnamo tarehe 27 machi 2005 mapande za saa 11 za magaribi.

Pascasie Nsimire ambaye ni mtoto wa bwana Chamunani, mkaaji wa tarafa la CANGENYI, mkoa wa Burhale katika mtaa wa Walungu aliweza kujeruhiwa vikali na risasi hiyo iliyomupita ndani ya shingo.

« Sans Blague » anatambulikana kama askari wa batayoni 52 ya Brigedi ya 5 ya FARDC iliyokuwa na makao huko Mulamba. Baada ya kutenda kitendo kile, imesemeka kama askari huyo amejielekeza sehemu za Kabare ambako kikosi chake kimetumwa na viongozi kwa ajili ya kuendelesha kazi. Binti Pascasie angali bado akilazwa kitandani mwa munganga katika hospitali kuu ya Walungu ambako anaendelea kufuata matunzo.
Wakaaji wa Burhale na pia raia wa Walungu ni wenyi kujiuliza kwa nini viongozi wa FARDC walimuachilia huru baada ya kujaribu kuondoa maisha ya binti yule bila sababu yoyote. Shida aliyopata Pascasie ni moja kati ya visa vingine vingi kuhusu ukiukaji wa haki za wanawake mtaani walungu ambazo RFDP hushurulikia mara kwa mara.

TUKIO MAALUM
MALALAMIKO YA WA MAMA WA WALUNGU

Ujumbe huu ulisomwa na mwakilishi wa Comité d’Alerte pour la Paix, CAP / Walungu. Ni kukundi cha kutetea amani ambacho kiliundwa na kinasindikizwa na shirika Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix. Ilikuwa huko mkoani Kaniola tarehe 4 machi 2005.

Mbele ya yote tuna sema jambo kwa wote. Tuna sema aksanti kwa vikundi vilivyo fikisha wakubwa wa FARDC na MONUC hapa kwetu Walungu nakutupatiya muda wakuweza kuzungumuza nao kwa sababu tulikuwa tunahitaji mkutano sawa huu tangu zamani.

Wandugu wapenzi,

Hatujuwe tuseme nini na tuache nini kuhusu maisha ya watu wa mtaa wa Walungu, hasa watu wa groupements Kaniola, Izege, Mulamba na Walungu. Tangu myaka 10 tunaishi na kutendewa sawa nyama za pori : Tunauwawa kiolela. Ni vigumu kujua idadi kwa kuwa ni nyingi. Tuna bebwa porini na kwenda ishi sawa watumwa. Tunabakwa na kubebeshwa ma mimba zisizo takiwa, tunaporwa mali, tunageuzwa uchuruzi : Kwani kuna beyi inakatiwa kwa watu walio bebwa porini. Beyi kwa mtu moja ni dolla 100 ili asiuwawe. Tunapata magonjwa za kuambukizwa kwa njia ya ubakaji, hasa Sida. Vitendo hivyo vinatendwa bila kuogopa sheria. Kwani hakuna hukumu wala malipizi kwa watenda maovu ile.
Wanawake wengi walitupiliwa na mabwana na jamaa zao nyuma ya kubakwa.

Kwa siku ya leo wanawake wa dunia nzima wanatayarisha sikukuu ya mama ulimwenguni. Lakini sisi wengine tunasambarana huku na huku tukigeuzwa wa « réfugiés » ndani ya inchi yetu.
Inabidi tujulishe MONUC kama sisi watu wa groupements Kaniola, Izege, Mulamba na Walungu tunaishi sawa sawa na watu wa Ituri, na yetu inatambuka kwa kuwa sisi tunagombanishwa na jeshi la inchi jirani. Tunaomba Communauté internationale yenye ilileta wanyarwanda mu Congo iwarudishe kwao Rwanda kwa kinguvu. Wazungu wajuwe kama na sisi tuko watu sawa wengine.

Tunashangalaka kusikia kama MONUC anakuwaka Walungu na iko pale kwa kusaidia watu kwa usalama wa Mtaa nzima ila tunatambua kama hahusike na maneno ile ndani ya mikoa za Kaniola, Izege, Mulamba na Walungu. Kama MONUC iko pale kweli juu yetu atiye watu wake wengi fasi zile zinazo gusiwa na kuangamizwa sana na wanyarwanda.

Wanapo sema uchaguzi mu Congo sisi tunashangaa sana. Maulizo nyingi inatupita kichwani :
Watu wa groupements zile wataenda je ku uchaguzi wakati wangali mu vita ya uvamizi ?
Utakuwa ulilala porini, unabakwa mbele ya bwana na watoto wako, tena watoto wale wabakwe nao mbele yako, muwe nyinyi wote wa « réfugiés », kisha utaenda jee kuchagua ?

Tunaliya na tunaomba mbele ya yote jeshi la Rwanda (milices rwandaises) yenyi kututesa iondoshwe kwa kingufu ndani ya mtaa wetu na kupelekwa kwao Rwanda na MONUC akisaidiwa na FARDC. Tunaomba Chapitre 7 ifanyike na iheshimishwe. Tunaomba uchunguzi na mafasiriyo kuhusu gari la mabawa lenyi kutuwa ndani ya pori ya Nindja (Cifuko na Lwizi).
Kwani tuna wasiwasi kwa sababu hatujuwe linatuwa nini na lina tuwiya nani.
Tunashanga na tuna jiuliza wa Nterahamwe wanatosha vifaa vya uzito vya vita wapi ?
TUKIO MAALUM

MALALAMIKO YA WA MAMA WA WALUNGU (… wa uk. wa 6)

MAOMBI YETU

1 MONUC na FARDC wasaidiane kwa kunyanganya silaha, kuondosha na kurudisha kwa kinguvu majeshi ya Rwanda (milices rwandaises) zenyi kupatikana kandokando na ndani ya pori ya Parc National ya Kahuzi Bièga mbele ya uchaguzi inchini mwetu.

2 Wahukumiwe na waazibiwe wale wote walio tenda vitendo vya ukahidi na vya ubakaji

3 Watu wote na MONUC wasaidiane kusudi sheria kuhusu ubakaji inayo kuwa sasa ndani ya Parlement ya Congo ikubaliwe

4 Monuc na Wakuu Viongozi wa Congo wagaramie jeshi la FARDC kwa vifaa vyenyi kutosha na vyenyi kustahili (silaha, mishahara, na vyakula) kwa ulinzi bora wa usalama katika mtaa wa Walungu

5 Communauté internationala ihukumu na kuazibu vikali kundi ya jeshi ya Rwanda (milices rwandaises) yenyi kutenda maovu mtaani Walungu, kwani ni wa terroristes

6 MONUC na FARDC watawanyishe jeshi zao kwa uwingi mahali popote inayovamiwa na majeshi za Rwanda, milices rwandaises

7 Waongozi na wakaaji wote wa mtaa wa Walungu waungane kwa kutambua, kutowa na kuazibu mkaaji yeyote anaye ambatana na kutumika pamoja na majeshi ya Rwanda yenyi kutuangamiza

8 Wakaaji wote wa mtaa wa Walungu, vikundi vya maendeleo na ma ONG washurulikie kwa namna zote wa hanga (mama na binti walio bakwa)

9 MONUC atusaidie kwa kuwarudisha mjini ndugu zetu wote walio bebwa porini. Wengi wako kule tangu siku za kutosha na wengine walipelekwa baadaye.

Ilifanyika pa Walungu, tarehe 3 Machi 2005

Wa mama wa mtaa wa Walungu (CAP/ Walungu)

Noella NDAGANO

Haki za wanawake ni pia
haki za binadamu

DOCUMENT

A l’occasion de la Journée Internationale de la Femme 2005

GLOBAL RIGHTS REND HOMMAGE A NEUF DEFENSEUSES DES DROITS HUMAINS PARMI LESQUELLES UNE DE LA RDC

« IL y a dix années écoulées que se tenait à Beijing (Chine) en 1995, la conférence mondiale sur les femmes. Cette quatrième du genre a été l’occasion pour la communauté internationale de s’engager à reconnaître entièrement les droits des femmes comme des droits humains .

Ces engagements sont regulièrement examinés par la Commission des Nations Unies sur le statut des femmes à New York.
A l’occasion de cette journée de la femme, au moment où le monde évalue le progrès réalisé dans la promotion des droits des femmes, il convient de rendre hommage à quelques femmes qui ont rendu ce progrès possible. Les neuf femmes que nous présentons ici et issues de nos organisations partenaires ont été sélectionnées en raison de leur activisme et de leur leadership. A travers leur force, leur vision et leur détermination, les droits humains des autres femmes et hommes sans voix ont connu une avancée ».

Cette citation est de l’Organisation Global Rights. Elle a été publiée à l’occasion de la Journée Internationale de la Femme, célébrée le 8 mars 2005. Cette ONG Internationale de défense et de promotion des droits humains en a profité pour présenter neuf femmes engagées dans la défense et la promotion des droits humains à travers le monde. Il s’agit de : Nilofar SAYAR (Afghanistan) Asma Charifi (Algerie ), Nusreta Sivac (Bosnie et Herzegovine ), Spès Caritas Ndironkeye (Burundi) ), Emiliana Lucia Bernard Stephenson (Colombie);Venantie BISIMWA (R.D.Congo), Mohini Chaudhary (India), Gulnahar Alam ( Etats Unis d’Amérique) et Maria Jose Fletcher des Etats Unis d’Amérique également.

Pour mémoire, Madame Venantie BISIMWA est la Secrétaire Exécutive du Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix , RFDP en sigle .
Elle est initiatrice et co-fondatrice de l’Association des Femmes Cadres pour l’Epanouissement Intégral de la Femme en 1992 et du Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix en 1999.

« Mama Vision » remercie Global Rights pour la reconnaissance du travail de ces défenseuses des droits humains et saisit cette opportunité pour encourager les lauréates d’aller de l’avant dans la protection et la promotion des droits humains.

(Pour plus d’information, veuillez visiter le site Internet de Global Rights :
http://www.globalrights.org)

Les droits des femmes sont aussi les droits humains

DOCUMENT

PROPOSITION D’UN PROJET DE LOI SUR LA REPRESSION DES VIOLENCES SEXUELLES EN RDCONGO

Il s’est tenu au centre Nganda de Kinshasa, du 2 au 4 mars 2005, un atelier national sur l’harmonisation de la proposition de loi pour la répression des crimes des violences sexuelles. Organisé par Global Rights en collaboration avec RAF (Réseau Action Femme), cet atelier a réuni 27 participants en majorité acteurs de la société civile issus de toutes les provinces de la RDC et intéressés à la problématique de violence sexuelle. Des représentants du Haut Commissariat aux Droits Humains et Human Rights Watch ont également pris part à ces assises.

Deux avant-projets de loi ont sanctionnés les travaux de Nganda :
1° La proposition de loi portant modification de certaines dispositions du code pénal, du code de procédure pénale et du code de la famille relative à la répression des infractions de violences sexuelles
2° La loi cadre portant création d’un fonds d’assistance aux victimes des infractions de violence sexuelle.

Ces deux textes ont servi de document de travail à un atelier similaire organisé à Iyonda à environ 15 km de la ville de Mbandaka et qui portait sur l’harmonisation de la législation congolaise relative aux violences sexuelles faites aux enfants, aux femmes et aux hommes.

Un deuxième atelier piloté par le FNUAP (Fonds des Nations Unies pour la population) et le HCDH (Haut Commissariat des Nations Unies pour les Droits de l’Homme) et qui s’était tenu du 9 au 15 mars avait été une occasion d’enrichir ces deux textes

Bulletin d’information du Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix, RFDP
72, av. Maniema, Ibanda, Bukavu, Sud-Kivu, RDC
Tel : +243 0813181854, +243 97783353
E-mail : rfdp1999@yahoo.fr

Edition n° 000 : spécial « Journée Internationale de la Femme 2005 »
Ont collaboré à cette édition

Venantie Bisimwa Nabintu, Rita Likirye, Laetitia Shindano Abel Bachishoga, Baciyunjuze Jean-Baptiste et Boniface Bahizire

N.B. Vos commentaires et suggestions sont les bien venus

SOCIETE
UNE FEMME COUTE 150$ A KANIOLA APRES PLUSIEURS NUITS DE VIOL ET VIOLENCES

‘’ C’était lundi à 20 heures, ils ont frappé violemment à la porte. Une voix très colérique nous obligeait à l’ouvrir de nous-mêmes si non… J’ai finalement ouvert, ils sont entrés avec fracas dans ma case. L’un parmi eux m’a pris par la main gauche, tandis que la main droite serrait contre ma poitrine mon bébé de deux mois. Il m’intima l’ordre de remettre l’enfant au lit et, d’un bond, il me tira dehors. Huit autres personnes capturées attendaient non loin de ma case, gardées par d’autres soldats RWANDAIS (entendez miliciens interhamwe et ou rastas) avec des armes braquées vers leur direction. Nos bourreaux étaient au nombre de 5, tous en uniforme militaire semblable à celui des congolais. Ils étaient lourdement armés et parlaient le kinyarwanda. Nous sommes conduits vers la forêt où nous avons rejoint d’autres groupes composés de nombreux hommes. En forêt, nous étions déplacés d’un lieu à un autre chaque nuit. . Nous étions battus selon le désir de celui qui nous approchait et j’étais, avec cette fillette ( elle indique du doigt une jeune fille, sa compagne du malheur, à peine âgée de dix ans) , violée plusieurs fois et par plusieurs personnes. Nous avions été relâchés ce matin pour récupérer la rançon de 900 $ exigés pour obtenir notre libération ainsi que celle de 5 autres otages restés en brousse. Ils nous ont prévenus qu’à défaut de cette somme d’argent, ils égorgeront nos compagnons restés en otage et entreprendront notre recherche par la suite pour nous faire subir le même sort que nos compagnons ».

Raconte une femme de 21 an d’âge dont nous taisons volontairement le nom, alors quelle revenait fraîchement de la forêt où elle avait été retenue pendant 6 jours et rendue esclave sexuelle par des éléments du FDLR - Interhamwe ou Rasta, ces combattants hutu rwandais qui sèment la mort et la désolation dans le territoire de Walungu. C’était, ironie du sort, à l’occasion de la journée de dialogue entre les femmes de Kaniola (Walungu ) et les autorités congolaises et celles de la MONUC( Mission des Nations Unies au Congo) organisé par le Réseau des Femmes pour la Défense des Droits et la Paix, RFDP. La préoccupation des femmes de Kaniola a consisté d’abord à exhorter la communauté internationale de désarmer et procéder au rapatriement rapide des combattants hutu chez eux pour que la paix revienne dans leur entité. Il s’agissait ensuite de demander que soient jugés, condamnés et punis de manière exemplaire tous les coupables des actes de viols et violences faites à la femme. C’est à ce motif que la femme de Kaniola pourra retrouver sa dignité et être ainsi en mesure de s’acquitter de ses devoirs civiques lors des prochaines élections à l’instar d’autres femmes et filles de notre pays.

Dans leurs revendications, les représentantes des femmes de Kaniola ont indiqué qu’au moins 2010 d’entre elles avaient été violées par des éléments du FDLR depuis 2003.
Selon leur dire, c’est chaque soir que ces bandits se déplacent des montagnes surplombant la contrée vers le village.

La pratique ancienne consistait en la recherche des denrées alimentaires, des ustenciles de cuisine, du bétail, ainsi que des femmes et les filles (celles-ci subissaient également des viols mais retournaient dans leur village après un certain temps). Actuellement, la pratique est devenue tout autre, regrettent- elles, ils viennent maintenant pour enlever hommes, femmes et enfants qu’ils torturent, violent et en tuent quelques uns pour enfin exiger une rançon contre la vie des survivants.

SOCIETE

UNE FEMME COUTE 150 DOLLARS A KANIOLA…(suite de la page 10)

Nous étions vendues à 100 dollars la personne. Il y a deux jours ce prix est passé à 150.Notre valeur humaine et notre dignité sont ainsi réduites en une simple marchandise, se plaignent-elles.

Cette petite contrée du territoire de walungu qui vient fatalement d’entrer dans l’histoire est une localité située à 12 kilomètres à l’ouest du chef-lieu du territoire. Elle abrîte 38.000 habitants. Parmi ceux-ci, 5.493 sont déplacés et actuellement vers Walungu-centre où nombreux parmi eux sont hebergés dans un camp de fortune érigé au stade Mafundwe. Kaniola est surplombé de collines ouvrant à la forêt où sont dissimilés les éléments hutus rwandais. Des scènes de prise d’otage, des rançons, des viols, des assassinats ,… sont la principale caractéristique de ces Rwandais basés a l’ouest et au sud – ouest de Walungu.

Budodo, cœur de cible ?

Ce village s’est vidé de ses habitants depuis le 19 février 2005. Monsieur Donatien Nakalonge, président du noyau de la société civile Walungu explique : « … dans la nuit du 27 au 28 août 2004, des miliciens FDLR /rasta ont envahi Budodo, en y emportant deux filles et 28 vaches. Dépassée par ces opérations à répétition et maintes fois dénoncées en vain, la population décide d’assurer sa protection en s’éloignant de Budodo.
Le terrain de football de Walungu dénommé Stade Mafundwe en reçut ainsi, le 1er septembre 2004 environ 1.170 ménages.

Cependant les exactions ne s’arrêtent pas là. Depuis ce jour, on signale 27 cas d’attaques dans ce petit village – avec une moyenne de 5 enlèvements par attaque - Au moins 14 personnes ont été tuées soit au village soit dans la brousse après enlèvement, 45 femmes et filles de tous âges violées et de milliers de dollars ont été ravis ou payés à titre de rançon.
« C’est à cause de l’ampleur de ces actes et du silence de l’autorité que la population a été contrainte d’abandonner cette terre où il faisait jadis beau vivre en choisissant l’exil », conclut notre interlocuteur.

Me Agathe RWANKUBA de retour à Bukavu

Me Agathe Rwankuba, membre du RFDP, est de retour à Bukavu en provenance de Yaoundé, Cameroun où elle a séjourné depuis le 15 décembre 2004.
Elle a été sélectionnée, au nom du Réseau des Femmes pour la Défense des Doits et la Paix, pour participer à un stage de 3 mois au Centre sous-régional des Nations Unies pour les Droits de l’Homme et la démocratie en Afrique Centrale.
Tout au long du stage, Me Agathe a développé deux thèmes à titre de participation :
- La sous - représentation de la femme dans les instances de prise de décision en Afrique Centrale. Elle l’a présenté comme une problèmatique à laquelle les Nations Unies doivent apporter une solution en faisant pression sur les Etats pour qu’ils puissent respecter les droits fondamentaux des femmes en général, et les droits civils et politiques en particulier.
- La situation des droits de l’homme au Tchad.
Mama Vision lui souhaite la bienvenue.
EVENEMENT
CRI D’ALARME DES FEMMES DU SUD-KIVU

A l’occasion de la commémoration de la Journée Internationale de la Femme 2005, les femmes de la province du Sud-Kivu regroupées au sein du CAUCUS DES FEMMES DU SUD-KIVU POUR LA PAIX ont rendu public un plaidoyer à l’intention de la communauté nationale et internationale.
Nous reproduisons le document in extenso compte tenu de l’importance du message de paix et de reconstruction nationale dont il est porteur.

PLAIDOYER DES FEMMES DU SUD-KIVU A L’OCCASION DE LA JOURNEE INTERNATIONALE DE LA FEMME DE L’AN 2005

Préambule

Nul n’ignore que depuis longtemps l’Etat congolais a failli à sa mission. Cela a occasionné l’avènement des guerres à répétition en général et l’entretien des zones de tension permanente en particulier. La femme, pourtant moteur de la survie familiale a toujours payé le lourd tribut en subissant des multiples exactions. Elle perd progressivement sa dignité et sa valeur jusqu’à sa chosification. De ces multiples exactions, notons les faits suivants :

A. Faits
Il est noté :

1. Par rapport aux viols et violences sexuelles faites à la femme

 Les détenteurs d’armes utilisent le viol comme arme de guerre,
 Les bandes armées étrangères violent et tuent les femmes qu’elles surprennent sur leur route, dans les champs et même dans leurs maisons. Le plus souvent, ces opérations sont bien planifiées et systématisées,
 Les bandes armées étrangères violent les femmes devant leurs enfants et leurs maris et donnent même lieu à l’inceste en exigeant les relations sexuelles entre parents et leurs enfants et vice versa,
 Les bandes armées étrangères emportent les femmes dans les forêts comme esclaves sexuels,
 Lors des événements de guerre provoqués par les dissidents Jules Mutebusti et Laurent Nkundabatware en mai et juin 2004 des viols systématiques ont été perpétrées sur la femme de la ville de Bukavu et environ
 Le harcèlement sexuel de la jeune fille dans les milieux universitaires et dans les écoles secondaires,
 La prostitution forcée chez les petites filles dans les maisons de tolérance,
 La sodomie des hommes rendant ainsi les ménages instables,
 Les criminels même découverts ne sont ni punis, ni inquiétés ou poursuivis,
 Nous déplorons le fait que même les FARDC sont entrain d’emboîter les pas aux armées étrangères dans leurs actions.
2. Par rapport à l’insécurité grandissante
 Les femmes sont devenues des réfugiés dans leur propre pays,
 Dans certaines parties des territoires du Sud-Kivu, les femmes ne passent pas la nuit dans leurs propres maisons,
 Les femmes sont devenues des portefaix d’armes,
EVENEMENT

PLAIDOYER DES FEMMES DU SUD-KIVU A L’OCCASION DE LA JOURNEE INTERNATIONALE …(suite de la page 12)

 L’accusation fortuite des hommes à l’endroit des femmes violées,
 Des tortures, des maisons incendiées par les bandes armées, des récoltes des champs des autochtones emportés, des pillages du bétail et autres objets de valeur entraînant la paupérisation totale de la population,
 L’insécurité dans les marchés ruraux,
 Des crépitements d’armes ça et là tandis que les hommes en uniformes qui continuent à insécuriser les gens dans la ville. Dans les milieux ruraux, les militaires sont beaucoup plus nombreux que les habitants,
 Les militaires démobilisés ou ceux qui se sont démobilisés d’eux même ne sont pris en charge pour leur réinsertion et pèsent ainsi sur les populations.

3. Par rapport à la faible participation des femmes dans la gestion de la chose publique

 Faible implication de la femme au processus électoral,
 Les femmes sont discriminées dans le milieu professionnel,
 Faible représentation de la femme dans les institutions de la transition en RD Congo,
 Les coutumes rétrogrades empêchent une participation massive des femmes dans la politique,
 Nombre élevé des pesanteurs qui empêchent à la femme de s’impliquer activement dans la gestion de la chose publique,
 Lourde chargée infligée à la femme,
 Les postes politiques et administratifs réservés à la femme sont fortement liés aux tâches traditionnelles lui imposées alors que les postes stratégiques sont exclus aux femmes.

B. LES RECOMMANDATIONS

Nous recommandons :

1. A l’ONU et autres intervenants internationaux

 La reconnaissance des viols et violences perpétrées sur la femme comme crime contre l’humanité

 Exiger à la MONUC d’appliquer le Chapitre 7 pour mettre hors d’état de nuire toutes ces bandes armées étrangères et les rapatrier dans leurs pays et ce, pour des fins de sécurité sur le territoire congolais et faciliter l’organisation des échéances électorales prochaines,

 La prise en compte par la Cour Pénale Internationale des exactions perpétrées depuis 1996,

 Faire pression sur le Gouvernement de la RD Congo afin que la parité homme-femme ressorte dans la constitution de la 3ème République,

 Que la MONUC revoie sa politique de DDR,

EVENEMENT

PLAIDOYER DES FEMMES DU SUD-KIVU A L’OCCASION DE LA JOURNEE INTERNATIONALE … (suite de la page 13)

2. Au Gouvernement de la RD Congo et aux autres acteurs nationaux

 De rétablir son autorité sur toute l’étendue du territoire congolais,

 Que dans le préambule de la nouvelle constitution dont se dotera la RD Congo soit mentionnée la convention sur l’élimination des toutes formes de discrimination à l’égard de la femme, ratifiée par la RD Congo,

 Que dans la nouvelle constitution la parité homme-femme ressorte et que des actions positives telles que le quota de 30 % soit non seulement instauré comme une mesure de bonne gouvernance et de démocratie mais aussi garanti aux femmes dans les prochaines institutions de la République,

 Que l’Etat congolais mette rapidement sur pieds un programme d’urgence de la prise en charge des femmes et filles victimes de viol et des violences sexuelles,

 Une fois identifiées, que les acteurs des crimes qualifiés soient poursuivis et condamnées pour purger leurs peines,

 Pour des cas de violences connus, adresser une pétition aux autorités compétentes pour que le jugement rapide soit fait et que cela serve d’exemple à tous.

 Que toutes les maisons de tolérance pour la prostitution de la fille mineure soient fermées et leurs propriétaires poursuivis en justice,

 Que les auteurs des harcèlements sexuels une fois identifiés soient chassés des milieux estudiantins et scolaires,

 Aux partis politiques de mettre en leur sein des mécanismes permettant une participation politique fructueuse de la femme congolaise compétente,

 Aux acteurs politiques responsabilisés dans les institutions de la transition de tenir leur promesse, entre autres, d’organiser en bonne et due forme les élections libres, démocratiques et transparentes possibles,

 Aux autorités politico-militaires et administratives de multiplier les efforts pour sécuriser tout le territoire national afin que l’organisation des élections soit possible à tous les niveauxA toutes les femmes congolaises et aux hommes épris de paix de militer pour que les pesanteurs internes et externes empêchent l’épanouissement global de la femme soient bannies.

Fait à Bukavu, le 08 mars 2005
Caucus Femmes du Sud-Kivu pour la paix